Nyumbani
16 Bora Shirikisho, mambo hadharani

BINGWA mtetezi wa Kombe la Shirikisho la CRDB, Yanga atacheza dhidi ya TMA Stars inayoshiriki Ligi ya Championship katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Katika michezo mingine, Simba watamenyana na Dodoma Jiji, huku Singida Black Stars wakicheza dhidi ya Mbeya City.
Matajiri wa Dar es Salaam, Azam watacheza na Fountain Gate, wakati Namungo watacheza na TRA United.
Kwa upande mwingine, Coastal Union watacheza dhidi ya Pamba Jiji, huku Geita Gold inayoshiriki Championship watakabiliana na Mashujaa.
Katika mchezo mwingine wa hatua hiyo, JKT Tanzania watapambana na Mbuni ya Championship.




