Kwingineko
Collins Sichanje ajiunga na klabu ya Charton Athletic

LONDON, UINGEREZA BEKI wa heshima wa soka la Kenya Collins Sichenje amefanikiwa kujiunga na klabu ya Charlton Athletic ya nchini Uingereza.
Sichanje amefanikiwa kiutia saini mkataba wa miaka miwili na nusu baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya FK Vojvodina ya nchini Serbia.
Hii ni hatua kubwa katika safari ya mchezaji huyo mwenye miaka 22, ambaye sasa ataanza kucheza katika Ligi ya Championship ambayo ni ligi daraja la pili la soka nchini Uingereza.
Sichenje amejiunga na Addicks akiwa ni rasmi mchezaji wa klabu hiyo kuanzia 2 Februari 2026, na amekuwa ni mchezaji wa saba katika usajili waliofanya timu ya Charlton katika dirisha la uhamisho la Januari hii.




