World Cup

Kombe la Dunia: Ghana yasahau jezi

Timu ya Taifa ya soka ya Ghana ‘Black Stars’ imekumbwa na aibu kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia 2022 mwezi huu Qatar baada ya kusahau jezi za michuano hiyo nchini mwao.

Michuano hiyo itaanza Novemba 20 na kumalizika Desemba 18.

Kwa mujibu wa ripoti ya African Press mratibu wa Black Stars alisahau jezi za timu hiyo nchini Ghana zitakazotumiwa na wachezaji wakati wa michuano hiyo kabla ya kuelekea Abu Dhabi, Muungano wa Falme za Kiarabu ambako imeweka kambi kabla ya kwenda Qatar.

Jezi hizo zitapelekwa Qatar kwa njia ya posta hadi kambi ya timu hiyo.

Licha ya kupata ufumbuzi wa tatizo hilo Chama cha Soka Ghana kina hofu kwamba jezi hizo huenda zisiwasili kabla ya mchezo wa kwanza wa Ghana kutokana na huduma duni za posta za Ghana.

Ghana ipo kundi H Kombe la Dunia pamoja na Ureno, Korea Kusini na Uruguay na mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Ureno Novemba 24.

Related Articles

Back to top button