Milan yaziba pengo la Reijnders

MILAN, MABINGWA wa zamani wa Serie A AC Milan wametangaza kumsajili kiungo wa Italia Samuele Ricci kutoka Torino kwa mkataba utakaomuweka Milan hadi Juni 2029 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Klabu hiyo haikuweka wazi taarifa za kifedha za usajili huo lakini vyombo vya habari vya Italia vinaripoti kwamba ada ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 iko karibu euro milioni 23.
Ricci ni zao la akademi ya Empoli, alihamia Torino mwaka 2022 na kufanikiwa kuichezea klabu hiyo mechi 113. Ameichezea timu ya taifa ya Italia mechi 10 tangu alipocheza kwa mara ya kwanza mwaka 2022.
Kuwasili kwa Ricci kunatarajiwa kuongeza afueni kwenye nafasi ya kiungo katika klabu hiyo kongwe ya jiji la Milan kufuatia kutimka kwa Tijjani Reijnders aliyejiunga na Manchester City




