Burudani

Gara B ataka serikali iwatambue

MSHEREHESHAJI wa matukio mbalimbali nchini Godfrey Deogratius Rugalabamu maarufu ‘Gara B’ ameliomba Baraza la Sanaa (BASATA) kuandaa mpango wa kufahamika rasmi washereheshaji ili pia watumike katika matukio ya kitaifa.

Akizungumza na SpotiLEO mapema hii leo, Gara B ambaye pia ni mwigizaji amesema ikibidi serikali iandae tuzo ambazo zitawatambua.

“Unajua tuko wengi sana Tanzania nzima na tunahudumia jamii kwa namna kubwa zaidi,” amesema Gara B.

Gara B ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha ‘Mr Right Show’ ameishukuru Serikali kwa kuweka mifumo mbalimbali katika maeneo mengi yanayowezesha urahisi wa utendaji kazi wao.

Mwigizaji huyo ambaye pia ni mjasiriamali amesema licha ya vipaji vyote alivyonavyo ila ameegemea zaidi kwenye ushereheshaji kutokana na wingi wa mahitaji.

Related Articles

Back to top button