50 Cent akataa bilioni 8 kutumbuiza kampeni za Trump

msanii wa Hip-hop nchini Marekani Curtis James Jackson ‘50 cent’ anadai kukataa kiasi cha pesa cha zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 8 ili kutumbuiza kwenye moja ya mikutano ya kampeni za mgombea urais wa marekani Donald Trump.
kupitia mahojiano yake na kipindi cha ‘breakfast club’ cha nchini Marekani, 50 cent amesema kuwa anaogopa sana kujihusisha na siasa pamoja na mambo ya dini kwani yanaleta mgawanyiko kwa watu na machafuko
“ni kweli nilipokea ofa ya kutumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za Trump kwenye ukumbi wa Madson Square Garden, lakini nilikataa kwa sababu zangu hasa mashabiki zangu. unajua naogopa sana siasa, ukijiingiza kwenye siasa lazima kuna wa kukupinga waibuke, sio wote watakubaliana na wewe. Naepuka siasa na dini, vitu hivi hasa dini ndivyo vilimgombanisha Kanye West na baadhi ya mashabiki zake. kiufupi mimi sipendi siasa”, amesema 50 cent.