Bushoke kulipwa milioni 500
Msanii wa Bongo Fleva Maximilian Luta Bushoke ameshinda kesi yake na kutakiwa kulipwa Sh. milioni 500 na Kampuni ya usambazaji wa kazi za wasanii inayojulikana kama Boomplay.
Mwanasheria wa Bushoke anayejulikana kwa jina la Clavery Mlowe amesema Mxcater kama muhusika Mkuu ndio aliyekuwa anapelekea kazi hizo Boomplay bila ridhaa ya msanii husika.
“Kisheria aliyepeleka kazi na aliyepokea kazi ya msanii bila ridhaa ya msanii husika wote wana makosa. Bushoke hajawai kupokea malipo ya kazi zake tangu 2018 wala kuchukua, hivyo wanapaswa kumlipa,”amesema Mlowe.
Mbali na hilo amemjibu msanii wa Hip hop Wakazi, baada ya kuhoji kuwa msanii Bushoke alikuwa anapost Instagram kuwa kazi zake zipo Boomplay na mwanasheria amejibu kuwa akaunti ya msanii Bushoke ilidukuliwa.
Ameongeza kuwa watuhumiwa wana nafasi ya kukata rufaa na pia sakata hilo lilianza muda kidogo na watahakikisha sehemu zote ambapo kazi za Bushoke zipo kinyume na sheria , wao wataenda kisheria zaidi kupata malipo ya kazi zake.