BundesligaKwingineko

Mashabiki wa United wanaumia! walitakaje?-Pogba

LONDON: KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba (31) amesema kwa sasa hana muda wa kuwafikiria mashetani hao badala yake ameelekeza nguvu zake kwenye kuyakabili matatizo yake na kujiandaa na namna atakavyorejea uwanjani.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 2018 ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na mtangazaji wa Sky Sports, Kaveh Solhekol aliyemuuliza iwapo angelitamani kukipiga tena ndani ya United au hata kuikumbuka ligi hiyo bora kwa sasa duniani.

“Kiukweli huwa natazama michezo ya Manchester kwa kuwa ina wachezaji kadhaa ambao tulicheza pamoja. Manchester ni klabu bora ulimwenguni,” ameeleza Pogba

Solhekol aliendelea kumchimba Pogba kwa kutaka kufahamu mtazamo wake namna ya mashabiki wa klabu hiyo wanavyopitia kipindi kigumu cha mateso kwa kupoteza makali yake uwanjani pia uhaba wa makombe.

“Ni kweli wanateseka. Kwani wanataka nini? Wanategemea nini?

“Binafsi siwezi kuizungumzia vibaya klabu iliyonilea na kuitumikia kwa uaminifu mkubwa. Huyo sio Paul, huyo sio mimi.

“United ina wachezaji wazuri, benchi bora la ufundi, pia ni klabu kubwa. Kwa sasa klabu inapambana kurudi kwenye ubora wake  na ninaamini itarudi katiba ubora kwa kuwa hali kama hii iliwahi kuwakumba Arsenal lakini sasa inawania ubingwa na ni klabu inavyofanya vyema Premier League sanjari na Manchester City hata Liverpool,” amejibu Pogba.

Mwezi Machi mwakani, Pogba anatarajiwa kurejea uwanjani akiwa na uzi wa Juventus kufuatia kufungiwa miaka minne kujihusisha na masuala ya soka baada ya kupimwa na kukutwa na kiwango kikubwa cha dawa ya dehydroepiandrosterone (DHEA) kabla ya adhabu hiyo kupunguzwa hadi miezi 18.

Related Articles

Back to top button