Yanga Vs Azam ni machinjioni Chamazi
MCHEZO wa Dar es Salaam Derby Yanga dhidi ya Azam FC, utapigwa Jumamosi, Novemba 2, Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi badala ya Benjamini Mkapa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Almas Kasongo amesema wengi walitamani mechi ichezwe Uwanja wa Benjamini Mkapa na kwakulitambua hilo waliwaandikia barua wamiliki wa uwanja huo isivyo bahati kutokana na maboresho yanayoendelea katika uwanja huo imeshindikana.
“Maombi yao hayakuweza kukubaliwa lakini unaweza kuelewa kwamba uwanja upo katika matengenezo makubwa na mkandarasi anahitaji muda zaidi na amepewa tarehe ya mwisho wa kukamilisha hiyo kazi kwa hiyo.
Imeonekana itakuwa changamoto ya kuweza kumsimamisha kutoendelea na hilo jambo kuwaruhusu Yanga. Kwa hiyo wamekataliwa tafsiri yake ni kwamba muda wa kikanuni kuwa wanaweza wakaenda nje, uwanja wao wa nyumbani unaweza usipate zile siku 21,” amesema Kasongo.
Amesema kwa hali hiyo kwa mujibu wa kanuni Yanga wanatakiwa kucheza uwanja wake wa nyumbani ambao ni Azam Complex bodi kwa kushirikiana na Yanga, wamiliki wa uwanja wako katika mazungumzo ya kupanga viingilio vya mchezo huo ili kuangalia takwimu za mashabiki watakaoingia kulingana na idadi ya uwanja.