Ligi Kuu
Azam FC mnawaelewa lakini?
DAR ES SALAAM; Azam FC ni kama wanacheza michezo yao ya Ligi Kuu kwa hesabu kali huku wakiendelea kupunguza mwanya wa alama baina yao na vinara Yanga.
Mpaka sasa matajiri hao wa kusini mwa Dar es Salaam wameshuka dimbani mara 22 wakiwa na alama 50 alama tano pungufu ya Yanga.
–
Azam sio tuu inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo bali pia ni timu ya pili uliyofunga mabao mengi kwenye ligi baada ya Yanga, kwenye uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa Azam wana wasatani wa mabao 33.
Mbali na hapo wachezaji wawili wa timu hiyo Feisal Salum pamoja na Kipre Junior kwa pamoja wamefunga mabao 21, Feisal akifunga 13 huku Kipre akiweka nyavuni mara nane.
Leo wakiwa Uwanja wa Azam Complex watawavaa Mashujaa FC ya Kigoma. Michezo mingine ya Ligi Kuu leo Geita Gold watakipiga na Wajelajela Tanzania Prisons, Tabora United Vs Kagera Sugar na Namungo FC Vs Coastal Union.