Ligi KuuNyumbani

Kikoti ni ‘Mwanamangushi’

KLABU ya Coastal Union ‘Wanamangushi’ ya Tanga, imenasa saini ya kiungo wa Namungo Lucas Kikoti kuitumikia timu hiyo ya Barabara ya 11 kwa mkataba wa miaka miwili.

Coastal Union pamoja na vilabu vingine vya Ligi Kuu Tanzania Bara ipo katika harakati za kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/2024.

“Sasa ni Mtakatifu wa Kaskazini…Lucas Almeida Kikoti ameweka gumba kuitumikia Coastal Union kwa miaka miwili,”imesema taarifa ya Coastal.

Wanamangushi hao hawakuwa na matokeo mazuri msimu uliopita licha ya kufanikiwa kusalia ligi kuu.

Kabla ya kujiunga na Namungo, Kikoti alikuwa akikipiga katika kikosi cha Maji Maji ya Songea.

Kikoti ni mchezaji wa pili kusajiliwa Coastal Union baada ya Ally Kombo aliyekuwa Ruvu Shooting.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button