BurudaniFilamu

Wema: Nimetimiza miezi 9 sijagusa pombe

DSM:Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amesema miongoni mwa vitu alivyofanikiwa mwaka huu ni kuacha pombe, kwani tangu Januari hajaigusa.

Akizungumza kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, Wema amesema mwaka huu ameona afanye sherehe kwani ni miaka mingi hajafurahia siku yake ya kuzaliwa.

“Sijasherekea siku yangu ya kuzaliwa siku nyingi, miaka kama 5, nafanyaga kawaida lakini leo ni tofauti nasherekea siku yangu ya kuzaliwa,mafanikio yangu kikubwa kuacha pombe, kwani ni vitu vingi nilivyopitia hadi nilipo sasa.

“Hakuna kitu kibaya kilichonikuta, nimeamua mwenyewe kwa kuwa tangu nianze kunywa pombe ni miaka mingi na haijanisaidia kitu chochote, ndo mana nimeacha natimiza miezi 9 tangu Januari nimeacha hadi leo, “amesema Wema na kuongeza kuwa mpenzi wake Whozu pia alichangia kumshawishi kuacha kwani alikuwa hapendi akimuona anakunywa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button