Burudani
Rubby na ndoto ya kolabo na Beyonce
DAR ES SALAAM:Malkia wa sauti Bongo, Hellen Majeshi, ‘Rubby’ anataka kufanya kazi na mrembo kutoka Marekani Boyonce kwa kuimba naye kiswahili.
Akiongea na Spotileo Rubby amesema, amejitahidi kupata wasanii wakali kutoka nchi mbalimbali katika albamu yake.
“Sijataka kuidondosha Tanzania yangu, watu wakae wakijua, hata wakisikia nimeenda kufanya ngoma na Beyonce na kwenye albamu ipo, msishangae mkanisikia nikiimba kiswahili mwanzo mwisho alafu kiingereza nikamwachia mwenyewe”.amesema Rubby