Wema amkana Idris Sultan hadharani

MTANDAONI: MUIGIZAJI wa Filamu nchini, ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amemjia juu Msanii wa Muziki Ommy Dimpoz baada ya kuchapisha maoni katika picha iliyopostiwa na Msanii Billnas aliyokuwa akimpongeza Idris Sultan kwa kushinda ($300,000) katika mashindano ya big brother yaliyofanyika nchini Afrika kusini mwaka 2011.
Dimpoz aliuliza “Hivi baada ya ushindi ndo akakutana na Wema Sepetu?” naye wema akamjibu “Sipendi ugomvi…sijawaji kula hata mia yake…yeye mwenyewe anajua”.
Leo katika ukurasa wa Instagram, Billnas ameposti picha ya Idris Sultan akiwa ameshika hundi ya Dola laki tatu alizowahi kushinda Big Brother aliyoambatanisha na maneno yasemayo
“Hongera sana Idris Sultani kipindi unashinda nilikuwa bado niko mwaka wa kwanza chuo sikuwa na simu…ila hongera sana kwa ushindi mkubwa sisi kama watanzania tunajivunia ushindi wako Taifa linajivunia vijana wenye uthubutu na ari ya kujituma kama wewe…wewe ni mfano wa kuigwa..”
Ikumbukwe kuwa Idris Sultan amewahi kuwa kwenye mahusiano na Wema kati ya mwaka 2015 na 2016, Lakini pia Billnas na Idris Sultan ni marafiki wakubwa na ni watu wenye utani mwingi hasa katika mitandao ya kijamii.