Filamu

Watoto wamuhuzunisha Brad Pitt

NEW YORK: MCHEZA sinema Brad Pitt ameelezwa kuwa na huzuni kubwa baada ya kushindwa kuwa na uhusisno wa karibu na mzuri na watoto wao yeye na mke wake wa zamani Angelina Jolie.

Watoto hao sita Maddox, Pax, Zahara, Shiloh, na mapacha Knox na Vivienne wana uhusiano mzuri na wakaribu na mama yao Angelina kuliko baba yao Brad Pitt.

Kwa mujibu wa ripoti ya US Weekly imeeleza kwamba mcheza sinema, huyo mwenye miaka 61 alikuwa na uhusiano usio na uhai na watoto wake wote sita hata kabla ya kutalikiana na mkewe licha ya kujaribu mara kadhaa kuwa weka karibu nao.

Chanzo kimoja kimeeleza kwamba ingawa Brad alijaribu mara kadhaa kuungana na watoto wake, bado hakuwa karibu na wengi wao, jambo ambalo linaonekana kumsababishia huzuni.

Kwa sasa, Brad hukutana na watoto wake wawili wa mwisho tu, Knox na Vivienne, mara moja moja. Uhusiano wake na watoto wake wengine, Maddox, Pax, Zahara na Shiloh, umezorota.

Kufikia sasa, Brad na Angelina wameendelea na maisha yao. Wakati mzee mwenye umri wa miaka 61, ambaye anajiandaa kwa ajili ya kutolewa kwa filamu yake ya mbio za magari ‘F1 The Movie’, sasa yuko kwenye uhusiano thabiti na Ines de Ramon, huku Angelina akidai kuweka mapenzi yake kwa watoto wao hao sita.

Brad na Angelina walipendana walipokuwa wakirekodi filamu yao ya ‘Mr. & Mrs. Smith.’ ya mwaka 2005. Mwaka 2014 walioana na 2016 wakaachana baada ya miaka miwili ya ndoa.

Walimaliza vita vyao vya talaka Desemba mwaka 2024 baada ya miaka minane kupita.

Related Articles

Back to top button