Watano washtakiwa kifo cha Liam Payne

ARGENTINA: WATU watano wamefunguliwa mashtaka nchini Argentina kuhusiana na kifo cha mwanamuziki Liam Payne, aliyefariki Oktoba 16, 2024 katika hoteli ya CasaSur huko Buenos Aires, nchini Argentina.
Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa, Jinai na Urekebishaji ya Argentina, imewataja walioshikiliwa ni meneja wa hoteli hiyo, ‘GAM’, aliyempokea alipofika nchini Argentina, ‘ERG’, na rafiki wa Payne ‘RLN’.
Taarifa hiyo imewataja Grassi na Roger Nores kwamba wameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya mwanamuziki Payne mwenye miaka 31 aliyekuwa katika kundi la One Direction kuanguka vibaya kutoka ghorofa ya tatu ya balcony ya hoteli hiyo.
Kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka, ‘EDP’, mfanyakazi wa hoteli, na ‘BNP’ mhudumu. Ezequiel Pereyra na Braian Paiz wameshtakiwa kwa kusambaza dawa za kulevya.
Kulingana na taarifa ya ofisi ya mwendesha mashtaka, ‘EDP’ anashukiwa kumuuzia Payne kokeini mnamo Oktoba 15 na Oktoba 16, huku ‘BNP’ akishukiwa kumuuzia kokeini mara mbili Oktoba 14.
Taarifa hiyo inasema ‘RLN’ amefunguliwa mashtaka ya kuua bila kukusudia baada ya kudaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa matunzo, usaidizi na usaidizi’ kwa Payne baada ya kumtelekeza akijua alikuwa na uraibu mwingi.
Pia ‘GAM’ anashtakiwa kwa kuua bila kukusudia kwa madai ya kushindwa kuzuia Payne asipelekwe kwenye chumba chake cha hoteli kabla ya kifo chake.
‘ERG’ ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia kwa madai ya kuwataka watu watatu kumburuta Payne, ambaye hakuweza kusimama peke yake, hadi chumbani kwake, badala ya kumuweka sehemu salama.
Kulingana na taarifa hiyo, Jaji Laura Bruniard amesogeza mbele mashtaka, ambayo mawakili wa washtakiwa wanaweza kukata rufaa. Hata hivyo, ikiwa rufaa zao hazitakubaliwa, kesi itaanza.
Kama RLN, GAM na ERG watapatikana na hatia watakabiliwa na kifungo cha mwaka mmoja hadi miaka mitano jela huku EDP na BNP wakikabiliwa na miaka minne hadi 5.
Mmoja wa washukiwa alikuwa “mtu ambaye aliandamana na msanii huyo kila siku wakati wa kukaa kwake katika jiji la Buenos Aires.” Mshukiwa wa pili alikuwa mfanyakazi wa hoteli anayeshutumiwa kwa kusambaza dawa aina ya kokeini, na wa tatu alidaiwa kumuuzia dawa za kulevya Payne.