Muziki

Kifo cha Liam Payne chakwamisha Netflix kuonyesha kipindi chake

NEW YORK: KIFO cha mwanamuziki Liam Payne kimeichelewesha Netflix kuonyesha kipindi kipya cha mwanamuziki huyo aliyekuwa akiimba katika kundi la muziki la One Direction.

Payne alikufa mapema mwezi huu akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tatu ya hoteli huko Buenos Aires.

Netflix walikamilisha kurekodi kipindi hicho cha ‘Building The Band’ na mkali huyo kuyoka One Direction miezi michache kabla ya kifo chake cha kusikitisha kutokea.

Netflix wameeleza kwamba Payne alifariki kabla haijapangwa tarehe ya uzinduzi wa mfululizo wa kipindi hicho: “Shirika litakutana na familia yake ili kujadili uwezekano wa kutolewa kipindi hicho katika siku zijazo.

Chanzo kimoja kiliiambia The Sun kwenye safu ya Bizarre kwamba “Ni mapema sana kufanya uamuzi, lakini onesho hakika halijasitishwa. Kipindi kilikamilishwa mwishoni mwa msimu wa joto. Netflix itakaa chini na familia ya Liam huu ni wakati sahihi kuzungumza juu ya safu hiyo na lini inaweza kutolewa.

“Kila mtu anayehusika amehuzunika na mioyo yao inaihurumia familia yake. Hakuna haraka au shinikizo la kutoa kipindi hicho wakati huu wa majonzi. Labda ingekuwa kipindi alipokuwa bora katika miezi kabla ya kifo chake.”

Liam alijipatia umaarufu pamoja na Niall Horan, Harry Styles, Louis Tomlinson na Zayn Malik na wakafanikiwa kupata mafanikio ya juu kabisa ya chati kama kundi la kwanza kutengeneza pesa nyingi duniani.

Lakini kundi hilo lilisitishwa mnamo 2016 na Liam alipata mtoto wa kiume Bear, saba, na mwenzi wake wa zamani Cheryl na kufurahia kazi ya peke yake na wimbo wake wa ‘Strip That Down’ na albamu yake pekee ya ‘LP1’.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button