“Wasanii mshindwe wenyewe”

DAR ES SALAAM: WASANII nchini huenda wakanufaika na mpango wa huduma ya bima za afya na bima ya maisha kwa wasanii wote nchini ambao unaendelea kujadiliwa baina ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA na kampuni ya Galco Insurance.
Imeripotiwa kuwa viongozi wa BASATA na kampuni ya Galco Insurance wamekutana na kufanya kikao hicho leo kujadili kuhusiana na mpango huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dk. Kedmon Mapana ameongoza kikao hicho na wajumbe wa Basata pamoja na Ugeni kutoka katika kampuni ya GALCO Insurance Brokers.
“Tumepokea Ugeni uliongozwa na Emmanuel Bugangu ambae ni Meneja wa kampuni ya Bima ya GALCO Insuarance Brokers akiwa na Ian Mmbando ambae ni Meneja wa Uendeshaji wa kampuni hiyo ambapo lengo la kikao hicho ilikuwa ni kutengeneza mpango wa ushirikiano wa utoaji wa bima za afya na bima ya maisha kwa wasanii nchini.”amesema Dk Mapana
Dk. Mapana amewapongeza GALCO Insurance Brokers kwa kuwa na mpango wa uwezeshaji mzuri wa upatikanaji wa huduma za Bima kwa Wasanii na kongeza kuwa Baraza la Sanaa la Taifa lipo tayari kushirikiana nao ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo kwa Wasanii nchini.
Aidha Meneja wa Kampuni hiyo Emmanuel Bugangu amesema kuwa lengo la mpango wa utoaji wa bima hizo kwa wasanii na wadau wa sanaa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wasanii na wadau wote wa sanaa.