Kwingineko

Wanaume badilikeni!, mnajichumia dhambi

MWIGIZAJI Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amewaomba wanaume kuacha tabia ya kuwatelekeza wanawake wanaozaa watoto walemavu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi baiskeli za walemavu, Steve amesema ulemavu sio ugonjwa ni changamoto ndogo inayotatuliwa.

“Wanaume wengi wamekuwa wakiwakimbia wake zao pindi wanapopata watoto walemavu jambo ambalo sio jema kwanini akizaliwa mzima unapenda mlemavu umkimbie nawaonya leo mwanzo na mwisho.”

“Leo Mama Ongea na mwanao tunakabidhi viti 250 pamoja na viatu  kwa watoto wahitaji wa watanzania walemavu ili kuwasaidia mama zao kuwapeleka shule tunawafuta jasho kwa hili wanapambana na watoto sana.”amesema Steve

Pia ameongeza kuwa hawataishia kwa Dar es Salaam bali wataenda mikoani pamoja na Pwani kusaidia kutoa viti kwa watoto walemavu kama sehemu ya kumsaidia mwanamke wa Kitanzania.

 

 

Related Articles

Back to top button