Kwingineko

Ishu ya kutumia dawa: Pogba avunja ukimya

UINGEREZA:Kiungo wa kati wa zamani wa kibibi kizee cha Turin Juventus Paul Pogba amevunja ukimya kuhusu sakata lake la kutumia dawa zilizopigwa marufuku mchezoni akikana kutumia dawa hizo kwa makusudi.

Pogba mwenye miaka 31 ameiambia Sky Sports UK katika mahojiano maalumu kuwa ni kweli alitumia dawa hizo lakini kwa mara nyingine amesema hakuwa anajua kuwa dawa hizo zinaongeza nguvu na zilipigwa marufuku kwa wanamichezo.

Pogba amesema dawa alizopewa zilikuwa virutubisho tu kama ambavyo mtu mwingine yeyote angetumia kwa ajili ya kuurutubisha mwili na hakulenga kusaidia jeraha lake kupona haraka au kumuongezea nguvu zaidi. Alipoulizwa ikiwa alikunywa dawa hizo ili awe ‘fiti’ Pogba alijibu “Hapana zilikuwa hazihusiani kabisa na majeraha niliyokuwa nayo wakati ule, wala sikunywa ili niwe fiti huo ndio ukweli. Vilikuwa virutubisho tu ambavyo mtu yeyote angemeza”

“Wanaonifahamu wanajua, walipoona jambo hilo walijua haikuwa makusudi, mimi ni mtu muaminifu sana, sio mdanganyifu. Ninaipenda kazi yangu na naupenda mpira, sipendi kudanganya napenda kushindana kwa haki. Kwangu ni bora kushindwa kuliko kufanya udanganyifu” amesema Pogba.

Ikumbukwe Pogba alifungiwa miaka minne kujihusisha na masuala ya soka baada ya kupimwa na kukutwa na kiwango kikubwa cha dawa ya dehydroepiandrosterone (DHEA) kabla ya adhabu hiyo kupunguzwa hadi miezi 18 akitarajiwa kurejea uwanjani na Juventus mwezi Machi 2025

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button