Nyumbani

‘Vyama vya michezo acheni migogoro’

DAR ES SALAAM: KATIBU  wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amevitaka vyama vya michezo kuongea lugha moja kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Amevitaka vyama hivyo kuachana na migogoro na kutumia mitandao ya kijamii kwa kusema mambo mazuri.

“Kwa sasa tuna uwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 na AFCON 2027. Viongozi wa vyama vya michezo kuepusha migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na kuepuka na taarifa mbaya za Taifa katika mitandao ya kijamii.

“Tukitumia mitandao kwa kuweka migogoro na kusambaza katika mitandao mambo ambayo yanayochochea uvunjaji wa amani basi hili suala la kupewa uwenyeji wa mashindano yatafutwa,” amesema.

Msigwa amesema tunapoenda kwenye uwekezaji mkubwa nchini inapaswa kuongea lugha moja kwa kuwa hakuna mwekezaji anayekuja kuweka fedha katika sehemu yenye migogoro

Related Articles

Back to top button