Uwoya aja na Kampeni ya “Jembe ni Mama”

DAR ES SALAM: MWIGIZAJI, Irene Uwoya, ametangaza kuwa Balozi wa Kilimo na kampeni yake ya kilimo, “Jembe ni Mama”, inayolenga kuwawezesha wanawake wa Tanzania kujikimu kupitia kilimo cha kisasa, kuongeza kipato, na kuboresha maisha yao.
Irene alieleza kuwa kilimo kimekuwa msingi wa mafanikio yake ya kiuchumi tangu aanze safari yake mwaka 2018, na sasa anataka kuhamasisha wanawake wengi zaidi kuwekeza katika sekta hii.
Irene amesema malengo ya kampeni hiyo ni kuimarisha ustawi wa wanawake kutambua nafasi muhimu ya wanawake katika kilimo na kuinua uchumi wa familia.
Teknolojia ya Kisasa: Kusaidia wakulima kutumia GPS, IoT, na kilimo cha akili kuongeza mavuno.
Kusaidia Wakulima Wadogo: Kuwapa pembejeo za kisasa, mikopo nafuu, na elimu ya kilimo bora.
Usawa wa Kijinsia: Kukuza nafasi ya wanawake katika maamuzi ya kifamilia yanayohusu mapato ya kilimo.
Miradi ya Kilimo:Irene amewekeza kwenye kilimo cha tangawizi (Mbeya), mpunga (Tanga), na tumbaku (Tabora).
“Jembe ni Mama Festival”: Nitamasha litakalo kuwa likifanyika kila mwaka litakalohamasisha kilimo cha kisasa na kusherehekea mafanikio ya wanawake wakulima.”
Aidha Irene Uwoya ametoa Wito kwa Wadau na serikali, mashirika, na wadau binafsi kushirikiana kufanikisha kampeni hii na amepongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha sekta ya kilimo.
“Mimi ni mwanamke, mama, na mkulima. Naamini kilimo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya taifa letu. Wanawake, tusimame imara, kwa sababu ‘Jembe ni Mama!’”amesema Irene Uwoya