UEFA champions league na sura mpya leo
Baada ya kusubiri muda mrefu hatumaye Ligi ya mabingwa barani Ulaya inarejea tena leo ikiwa na sura na muundo mpya wa uchezaji.
Mfumo wa zamani wa hatua ya makundi umeondolewa na sasa mfumo mpya wa Ligi yenye timu 36 utaanza leo hii. Ambapo tayari kila timu imeshafahamu ni nani itaenda kucheza nae katika mfumo huu ambao unatarajiwa kuwa na msimamo wa ligi.
Kila timu katika mfumo huu itacheza mechi 8 yaani nne nyumbani na nne ugenini kwa UCL yenyewe na UEFA Europa league. kwenye UEFA Conference league kila timu itacheza mechi sita.
Timu zitakazomaliza hatua hii katika nafasi 8 za juu zitaenda moja kwa moja kwenye hatua ya 16 bora. Timu zitakazomaliza nafasi ya 9 hadi 24 zitacheza Playoff ili kupata timu nyingine 8 za kuungana na 8 za awali. Zitakazomaliza nafasi ya 25 hadi 36 zitaondoshwa moja kwa moja kwenye mashindano.
Kuanzia hatua ya 16 bora kila mechi itachezwa nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasonga hatua inayofuata.
Mechi za leo, Septemba 17
Juventus vs PSV Eindhoven – 19:45
Young Boys vs Aston Villa – 1945
AC Milan vs Liverpool – 22:00
Bayern Munich vs Dynamo Zagreb – 22:00
Real Madrid vs VfB Stuttgart – 22:00
Sporting CP vs Lille – 22:00