Twiga Stars kambini Sept 7

WACHEZAJI 27 wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ kitakachoingia kambini Septemba 7, 2023.
Kikosi hicho kitaingia kambini kujiandaa na michuano ya ubingwa wa Afrika wa soka la Wanawake itakayofanyika Morocco 2024.
Wachezaji walioitwa watakaokuwa chini ya Kocha Bakari Shime ni Najat Abasi, Zulfa Makau, Husna Mtunda, Juletha Singano, Anastazia Katunzi, Happy Hezron na Christer Bahera.
Wengine ni Vaileth Nicholaus, Fatuma Issa, Joyce Lema, Diana Lucas, Noela Luhala, Aisha Juma na Zainabu Mohamed.
Wachezaji wengine wa kikosi hicho ni Janeth Pangamwene, Koku Kipanga, Amina Ally, Donisia Minja, Enekia Kasonga na Stumai Abdalah.
Wengine walioitwa ni Diana Mnali, Sarah Joel, Ester Mabanza, Aisha Masaka, Oppa Clement, Jamila Rajabu na Winfrida Gerald.