Burudani

Mobotto mimi na Aziz Ki tupo hivi….

Baada ya Hamisa Mobetto kuhusishwa na nyota wa Yanga, Azizi Ki kubaki klabuni hapo, mwanamitindo huyo amevunja ukimya juu ya sakata hilo.

Amesema picha na video zinazoendelea katika mitandao ya kijamii kati yake na Mchezaji wa Yanga Aziz Ki ni kwasababu wawili hao ni marafiki wa karibu sana.

“Nilimwambia Azizi Ki asiondoke ndio mana niliandika maneno kama angeondoka ingekuwaje? na kama Azizi Ki angeondoka ningepanda ndege kumfuata popote alipo.”amesema Hamisa

Hamisa amesema Azizi Ki ni mchezaji mzuri  kama mnavyojua ameongoza kwenye ligi kuu.

“Binafsi sikufuatwa na mtu yoyote kumshawishi Azizi Ki kubaki bali nilimsahuri na yeye ameamua mwenyewe ukizingatia ni mchezaji mzuri anastahili kuendelea kucheza katika timu hiyo.

“Ni marafiki wa karibu sana kiasi kwamba asingeweza kuindoka na kumuacha.”

Pia ameongeza kuwa endapo Azizi Ki angeondoka Tanzania angemfata huko huko alipo asinge mwacha.

 

Related Articles

Back to top button