Burudani

Diamond: Ukishindwa kutoboa basi tena

DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Wasafi Nassibu Abdul ‘Diamond platnumz’ amesema ikitokea awamu hii mtu akishindwa kutoboa basi asilaumu serikali.

Akizungumza Dar es Salaam katika hafla ya Iftar aliyoiandaa kwa wadau mbalimbali wa sanaa Diamond amesema kwa sasa mambo yamefunguka na kuna fursa nyingi zilizotengenezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Fursa ni nyingi, mambo yamefunguka na ufanisi umekuwa mkubwa. Tumepata Rais ambaye ana huruma na ubinadamu ndani yake, ana roho nzuri anajitahidi kuhakikisha hakuna deni, kama ni deni basi tutabaki nalo sisi,”amesema.

Amesema: “Nikiwa kama mmoja wa vijana wa Kitanzania ukiniletea fursa naondoka nayo,”amesema.

Diamond alitumia nafasi hiyo kutambulisha bidhaa mpya ya sabuni chini ya Wasafi ikiwa ni miongoni mwa fursa zitakazowapa vijana wengi ajira.

Baraza la Sanaa la Taifa Basata lilimpongeza Diamond kwa hatua hiyo kubwa na ya kipekee katika kupanua wigo wa ubunifu wake nje ya muziki.

“Hatua hii pia ni ushuhuda wa kujituma na ubunifu wa hali ya juu kutoka kwa msanii huyo ambaye ameendelea kuonesha mfano bora kwa wasanii wengine nchini na nje ya mipaka,” imesema taarifa y Basata.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button