Kuogelea

TSA yaingia makubaliano na Great Lakes

DAR ES SALAAM: Chama cha kuogelea Tanzania TSA kimeingia makubaliano na kampuni ya Great Lakes kudhamini timu ya taifa ya kuogelea itakayoshiriki mashindano ya Africa Aquatics kanda ya tatu Bujumbura nchini Burundi kuanzia Novemba 22 mpaka 24.

Kwa mujibu wa Msemaji wa TSA Sebastian Kolowa, Great lakes wametoa shilingi milioni 4.48 ambayo itatumika katika safari hiyo.

“TSA inaendelea kuwaomba wadau wengine kutoka tasnia na makampuni mbalimbali kuendelea kuipa nguvu timu yetu hii ili turejee na ushindi,”amesema.

Amesema fedha hizo watapewa wachezaji ziwasaidie katika safari yao na kuhakikisha wanakwenda kupambana kwa kujitoa na kurudi na medali nyingi.

Kolowa amesema timu ya wachezaji 39 imeanza maandalizi ya michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button