Burudani
Tessy autaka muziki

Mrembo Tessy chocolate anasema tutarajie siku moja kumuona akiingia Studio na kuachia ngoma yake.
Akipiga Story na spoti leo Tessy anadai mwili aliokuwa nao mwanzo ulimkwamisha kufanya vitu vingi lakini kwasasa yuko sawa na anafanya vitu vingi sana.
“Mwili wangu wa awali ulinikwamisha kufanya vitu vingi lakini kwa sasa mtarajie mengi kutoka kwangu ikowemo kuimba na kucheza.”
Tessy ameongeza kuwa siku hizi ameingia kwenye Tasnia ya uigizaji na anaweza akaonekana kwenye Music Video ya msanii yeyote yule kama akifuata vitu anavovihitaji na hata ikitokea ni Baba Mtoto wake Aslayisihaka itifaki lazima izingatiwe.