Tems uso kwa uso na Beyonce

CALIFORNIA: VIPENGELE vya Tuzo za Grammy 2027 vimetangazwa na jina la Mnigeria, Tems limechomoza kwenye kipengele muhimu cha Best R&B Solo Perfomance.
Kwenye kipengele hicho, Tems atawania dhidi ya wakali Beyonce, Kehlani, Victoria Monet na Jill Scott.
Tems pia anawania kipengele kingine cha Best Global Music Album kupitia albamu yake ya Love Is A Kingdom dhidi Ayra Starr (Star Girl), Davido (Oriade), EQUILIBRIVM (Anitta) na Hope!! ya Angelique Kidjo.
Aidha, mkongwe Kidjo pia amepenya kuwania kipengele cha Best African Music Perfomance kwa Wimbo wa Aye Kan aliomshirikisha Ayra Starr.
Na wengine anaowania nao katika kipengele hicho ni Wizkid & Asake (Jogodo), King Ayisoba & Rocky Dawuni (No Tradition, No Africa) na mwisho ni Asake kupitia Wimbo wa Gratitude.
Hafla ya utolewaji wa tuzo hizo inatarajia kufanyika Februari 7, mwakani kwenye Arena ya Crypto.com, Los Angeles.




