AFCON

TASWA: Heko Taifa Stars

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimetoa pongezi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, wasaidizi wake na wachezaji wa Taifa Stars kwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2025 nchini Morocco.

Taarifa ya TASWA iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Imani Makongoro imewapongeza pia wananchi waliofurika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuiunga mkono Taifa Stars kwa dhati na kuwapa hamasa wachezaji mwanzo hadi mwisho wa mchezo mgumu tulipopambana na Guinea na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 Novemba 19, 2024.

“Tunawasihi Watanzania tuendelee kuiunga mkono Taifa Stars, kwani safari bado ni ngumu na ndefu. Ni vizuri kwa mshikamano ambao tumeonesha hadi tukafanikiwa kuvuka kizingiti na kupata tiketi ya kwenda Morocco tukauendeleza kwa kasi zaidi“, imeeleza taarifa hiyo na kuongeza

“Tunaomba matayarisho kwa fainali za mwakani yaanze mara moja na kila mwenye uwezo ajitokeze kuisaidia Taifa Stars, kwani ushindi wao ni wa kulijengea heshima Taifa letu. Kwa pamoja tutashinda. Heko Taifa Stars.

Related Articles

Back to top button