Africa
Che Malone aiangukia Simba

DAR ES SALAAM: MLINZI wa Simba SC, Che Malone Fondoh amewaomba radhi viongozi, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kwa makosa ya kujirudia uwanjani.
Katika maelezo yake kupitia akaunti yake ya Instagram, Malone amesema anajutia na kuumizwa kwa kuiigharimu timu katika michezo miwili na kuahidi kuyafanyia kazi makosa yake ili kuwa bora.
Katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa jana, Che alifanya makosa yaliyosababisha mnyama kufungwa baada ya kutoa pasi fupi iliyonaswa na mshambuliaji wa FC Bravos kabla ya baadae mnyama kuchomoa kipindi cha pili na kufanya ubao kusoma 1-1.