Michezo Mingine

Tanzania Kriketi bingwa wa kanda

TIMU ya taifa ya Kriketi imeibuka bingwa wa michuano ya kanda ya Afrika kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuichapa Malawi kwa mikimbio 19.

Katika mchezo huo wa kuhitimisha hatua ya makundi kundi A, Tanzania na Malawi zilizokuwa zikilingana pointi nane awali, zilicheza mchezo wa fainali kwa ajili ya kupata bingwa wa kanda.

Ushindi huo uliifanya Tanzania kuibuka bingwa wa kundi hilo kwa kufikisha pointi 10, huku Malawi nane, Ghana sita, Cameroon nne, Lesotho mbili huku Mali ikishika mkia ikiwa haina pointi.

Tanzania na Malawi zimefuzu hatua ya pili tayari hivyo, zitakutana na timu nyingine sita kwenye makundi mengine kucheza hatua ya mtoano kupata timu mbili zitakazowakilisha Afrika katika fainali za dunia hapo baadaye.

Wachezaji bora wa mashindano hayo ni Sami Sohail aliyefunga jumla ya mikimbio 137, akifuatiwa na Suhail Vayani mwenye wiketi 13 wote wa Malawi, mchezaji bora wa mashindano ni Obed Harvey wa Ghana na mchezaji bora wa mechi hiyo ni Khalidy Amir.

Related Articles

Back to top button