Muziki

Stevie Wonder, John Legend, Chris Martin, kutumbuiza Grammys 2025

LOS ANGELES: AKAUNTI rasmi ya Tuzo za Grammy imelithibitisha kwamba wasanii Stevie Wonder, John Legend na Chris Martin wa Coldplay watakuwa miongoni mwa watumbuizaji katika tuzo za waigizaji kwenye GRAMMYs zitakazofanyika Februari 2 mwaka huu 2025.

Wasanii wengine watakaotumbuiza katika siku hiyo ni Cynthia Erivo, Lainey Wilson, Herbie Hancock, Brittany Howard, Brad Paisley, Janelle Monáe, Sheryl Crow, St. Vincent na Jacob Collier.

Wengine ni Benson Boone, Billie Eilish, Chappell Roan, Charli XCX, Doechii, Raye, Sabrina Carpenter, Shakira na Teddy Swims.

Sherehe za usiku wa tuzo hizo unatarajiwa kuwa wa tofauti kutokana na mfululizo wa maonesho maalum yaliyopangwa ikiwemo utoaji wa heshima kwa Quincy Jones,

Wasanii waliopangwa kuanza maonesho yao ni Yolanda Adams, Wayne Brady, Deborah Cox, Scott Hoying, Angelique Kidjo, na Taj Mahal, pamoja na Joe Bonamassa, Joyce DiDonato, Béla Fleck, Renée Fleming, Muni Long, na Kelli. O’Hara, Bob Clearmountain, Rhiannon Giddens, Malkia Sheba, Anoushka Shankar na Jimmy Jam.

Related Articles

Back to top button