Muziki

Ed Sheeran, ziarani miji 6 nchini India

NEW DELHI: MWANAMUZIKI wa Uingereza Ed Sheeran yupo katika ziara ya miji sita nchini India kuanzia jana ambapo alifanya onesho la nguvu katika mji wa Pune.

Ed Sheeran alipanda jukwaani akiwa amevalia fulana iliyoandikwa ‘Pune’ akisherehekea na umati uliolipuka kwa furaha!

Sheeran alisema ameimba mara mbili nchini India, mara zote mbili huko Mumbai na alifurahi kuleta muziki wake katika miji mingine nchini India. Pia alieleza kuwa kila ziara humfanya ajisikie kama mtalii anayetembelea nchi nzuri na kwamba daima anashukuru kwa fursa ya kutumbuiza watu wa India.

Ziara ya Mwanamuziki huyo nchini India inatolewa na kukuzwa na AEG Presents Asia na BookMyShow Live,kwa mujibu wa kampuni hiyo Ed Sheeran atatumbuiza katika mji wa Hyderabad, Chennai, Bengaluru, Shillong na Delhi-NCR.

Ed Sheeran amekuwa akijizolea wafuasi wengi kutokana na aina ya muziki anaofanya hasa akiwavutia wanawake kwa upigaji wake wa gitaa na kuimba nyimbo za mapenzi zenye jumbe mahususi kwao

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button