“Stars iko vizuri kupambana na yoyote AFCON”

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Timu ya Tanzania Taifa Stars, Hemed Sulemani ‘Moroco’, amesema anaimani na Stars kufanya vizuri na kuvuka hatua ya makundi ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 itakayofanyika nchini Morocco.
Tanzania imepangwa kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda kwa ajili ya fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.
Morocco amesema kundi sio jepesi, timu zilizofuzu katika hatua hi izote nzuri, zina ubora, suala lililopo ni kufanya maandalizi mapema na kuwaheshimu wapinzani walipo kundi hilo.
“Timu ikishafuzu katika fainali za AFCON unakubali hali yoyote ambayo unakutana nayo, unahitaji ucheze nao. Hakuna kundi jepesi timu zote zimefanya vizuri na kufuzu.
Tumepokea tunahitaji kujipanga kwa sasa , tuheshimu kila mmoja kwenye kundi letu kwa jinsi tulivyo sasa hivi tuko vizuri tunaweza kupambana na timu yoyote,” amesema.
Kocha huyo amesema wanatakiwa kufanya maandalizi ya michuano hiyo mapema, kwa sababu anatambua timu wanazoekutana nazo sio ngeni baadhi wamekutana ikiwemo Uganda wakionyeshana ubabe.