AFCONAfrica

Ni nusu fainali ya kibabe AFCON

NUSU fainali ya michuano ya 34 ya Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) inapigwa leo huko Ivory Coast.

Nigeria iliyotwaa taji hilo mwaka 1980, 1994 na 2013 itaikabili Afrika Kusini iliyoshinda 1996 kwenye uwanja wa Stade Alassane Ouattara uliopo Kaskazini mwa jiji la Abidjan.

Katika nusu fainali ya pili wenyeji Ivory Coast waliotwaa kombe hilo mwaka 1992 na 2015 itachuana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliyokuwa bingwa mwaka 1968 na 1974 kwenye uwanja wa La Paix uliopo jiji la Bouaké.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button