Staa wa Hollywood Liam Neeson kustaafu kucheza filamu mwakani 2025
NEW YORK:NYOTA wa filamu ya ‘Taken’ iliyotoka kwama 2008, Liam Neeson amesema siku zake za kucheza filamu za mapigano zinakaribia kuisha, hivyo anataka kustaafu mapema kabla hajapoteza ushawishi kwa mashabiki wake.
Nyota huyo wa Hollywood mwenye miaka 72 amesema kuna wakati utafika hatoweza kupiga ngumi kama anavyofanya sasa huku akiweka wazi kwamba huenda mwishoni mwa mwakani atastaafu rasmi kucheza filamu.
Alisema: “Nina umri wa miaka 72 lazima ifike mwisho katika hatua fulani. Huwezi kudanganya watazamaji na sitaki mshirika wangu wa muda mrefu Mark Vanselow awe anacheza sehemu za mapigano ninayopaswa kucheza mimi.
Liam aliendelea kuweka wazi kwamba atastaafu kucheza sinema zake: “Labda mwisho wa mwaka ujao. Nadhani ndivyo hivyo nitastaafu.”
Muigizaji huyo anatazamiwa kuonyesha uwezo wake mwingine wa kuchekesha katika filamu yake inayofuata ya ‘The Naked Gun’ lakini hana uhakika kama atabadilisha hatua kutoka kucheza filamu za mapigano hadi kucheza filamu za kuchekesha siku zijazo.