Ligi Kuu

Simba morali juu kuelekea debi

DAR ES SALAAM: MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi hicho kimerejea salama na kinaendelea na kambi ya ndani huku maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga yakizidi kushika kasi.

Akizungumza Dar es Salaam Ahmed amesema morali ndani ya kikosi hicho ni kubwa kutokana na timu kuanza vizuri msimu wa Ligi Kuu, huku wakilenga kuendeleza mwenendo huo katika mchezo huo wa watani wa jadi utakaochezwa Oktoba 10 kwenye Uwanja wa Uhuru.

“Kwa upande wetu Simba tumerejea salama. Tunaendelea na kambi ya ndani kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga. Morali ni kubwa sana, ligi tumeanza vizuri, tunataka kuwa na mwendelezo mzuri,” amesema Ahmed.

Amesema mchezo huo utakuwa kipimo muhimu kwa timu yao kutokana na ubora wa wapinzani, akisisitiza kuwa Simba ina kikosi kinachoweza kushindana katika mchezo huo.

“Simba dhidi ya Yanga tunaenda kupata ubora wa hali ya juu. Tuna timu bora ya kushindana, kipimo ni mechi ya tarehe 10,” amesema.
Ahmed pia amesema licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa ya mvua kipindi hiki anaamini kikosi hicho kitakuwa katika hali nzuri kuelekea mchezo huo wa Oktoba 10.

Related Articles

Back to top button