Muziki

Sean Paul afunguka kuhusu mke wa Jay Z

Los Angeles, MAREKANI: BAADA ya miaka 21 kupita mkali wa dancehall kutoka Jamaica Sean Paul, amefunguka jinsi alivyoimba wimbo wa ‘Baby Boy’ ambao alishirikishwa na mke wa rapa mashuhuri nchini Marekani Shawn Carter (Jay Z), Beyonce Knowles.

Beyonce ambaye ni mwimbaji wa pop wa Marekani alimshirikisha Sean Paul kwenye wimbo huo wa ‘Baby Boy’ kutoka kwenye albamu yake ya 2003 ya ‘Dangerous Love’ ambao hadi sasa video ya wimbo huo kwa Youtube inawatazamaji zaidi ya milioni 206.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na The Hollywood Reporter, Paul alibainisha kuwa kabla ya kushirikiana katika wimbo huo Beyoncé aliacha starehe zote alizokuwa akifanya wakati huo akaenda alikotakiwa kufika kwa ajili ya kolabo ya wimbo huo uliofungua nji kwa muziki wa dancehall kukubalika duniani kote na kuweka historia kwa wanamuziki hao wawili.

“Nilikuwa nikifanya kazi na Busta Rhymes, Blu Cantrell na hao wote walikuwa wanamuziki wa hip-hop na kipindi hicho Beyoncé alikuwa anapitia katika njia zake,” alieleza Sean Paul.

Sean Paul alisema baa da ya wimbo huo akatambua kuwa muziki wake wa dancehall ulikuwa ukikubalika mno duniani kote.

“Wakati huo nilikuwa nimetokea Texas na najua amekuwa akisikia nyimbo nyingi za dancehall kipindi hicho lakini alinichagua tukafanya wimbo ukaenda ni heshima kwangu kufanya wimbo ule na Beyonce ndiyo uliofungua njia kwa muziki wa dancehall na umetengeneza historia kwetu sote,” alieleza Sean Paul.

Sean Paul Ryan Francis Henriques amezaliwa Januari 09, 1973 albamu yake ya kwanza ‘Stage One’ aliitoa mwaka 2000, mwaka 2002 alitoa albamu nyingine aliyoiita ‘Dutty Rock’ na baada yah apo alianza kuachia nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikifanya vizuri katika chati mbalimbali za muziki.

Related Articles

Back to top button