Kwingineko
Ronaldo mfalme wa rekodi?

CRISTIANO Ronaldo ameandika historia nyingine kwenye soka ulimwenguni baada ya kuwa mchezaji mwanaume aliyecheza michezo mingi zaidi timu ya taifa.
Ronaldo leo Juni 20 amecheza mchezo wake wa 200 akiwa na Ureno kwenye mchezo wa kuisaka tiketi ya michuano ya mataifa ya Ulaya mwaka 2024 dhidi ya Iceland na kuandika historia mpya kwenye soka la Ureno na ulimwenguni kwa Ujumla.
Rekodi hiyo imemfanya nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno kuingia kwenye kitabu cha rekodi za kipekee ( Guinnes World Records book)
Ronaldo amekikipiga timu ya taifa ya Ureno kwa zaidi ya miaka 20 tangu alipoanza Agost 2003 hadi sasa.