FA

Ramovic awatingisha Copco

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema atatumia mchezo wa kesho hatua ya 64 ya kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Copco FC kama daraja la kutetea ubingwa wa michuano hiyo.

Yanga itashuka dimba la KMC kusaka ushindi dhidi ya wapinzani hao kutoka mkoani Mwanza.

Kuelekea mchezohuo Kocha wa Yanga, Sead Ramovic, amesema kuna baadhi ya wachezaji watakosekana kutokana na kuumwa lakini waliokuwepo wapo tayari kwa mchezo wa kesho, lengo ni kushinda dhidi ya Copco ikiwa sehemu ya kuanza safari ya kutetea ubingwa.

“Sio kwamba tuna wachezaji 11 bora wa kikosi cha Yanga bali wachezaji wote 25 ni bora na wako tayari kwa mechi ya kesho,” amesema.

Kocha wa Copco FC, Lucas Mligwa amesema wamejiandaa vizuri kuwakabili Yanga, wamekuja na malengo na watahakikisha yanatimia kupitia mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.

“Tumekuja kucheza tukiamini Yanga ni bora, tunajua uwezo mkubwa na ubora wa wachezaji wao kuliko sisi, ukiangalia mchezaji mmoja mmoja tofauti na wachezaji wangu.

Mipango yetu ni kupunguza eneo la kucheza kama wanakuwa bora basi sisi tutakuwa na namba kubwa uwanjani, tukifanya hivyo ninaimani mipango yetu itaenda vizuri,” amesema.

Kocha huyo amesema licha ya kiufundi lakini pia amekaa na wachezaji wake kuwajenga kisaikolojia kwa sababu wanakutana na timu kubwa na wachezaji wenye ubora zaidi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button