Mitindo

Prisca Lyimo kupeperusha bendera ya Tanzania Miss Cosmo 2026

DAR ES SALAAM: BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaomba Watanzania, wadau wa sanaa, mashabiki wa mashindano ya urembo na jamii kwa ujumla kumuunga mkono mrembo Prisca Lyimo anayewakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Cosmo 2026.

Akizungumza na Spoti leo Mkurugenzi Msaidizi Sanaa za Ufundi na maonyeshokutoka BASATA, Bona Masenge

amesema ushiriki wa Prisca katika mashindano hayo ni fursa muhimu ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vipaji, ubunifu na utambulisho wa taifa.

Kupitia wito huo, baraza hilo limewahimiza “Watanzania kuungana kumtia moyo mrembo huyo na kufuatilia safari yake katika mashindano hayo ili kumpa nguvu na kumwezesha kuwakilisha vyema nchi.

“Mtanzania mwenzetu, Prisca Lyimo, anaiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Miss Cosmo 2026. Hii ni fursa ya kuonesha vipaji, ubunifu na utambulisho wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa,” ameeleza

Aidha Bona amewataka Watanzania kuonesha mshikamano kwa kumuunga mkono Prisca katika safari yake hiyo, likisisitiza umuhimu wa kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia majukwaa ya kimataifa.

“Tushikamane, tumpe nguvu na tuendelee kuipeperusha bendera ya Tanzania!” imesisitiza .

Wito huo unaonesha umuhimu wa mshikamano wa Watanzania katika kuwaunga mkono wawakilishi wa nchi katika mashindano ya kimataifa, ambayo hutoa fursa ya kutangaza utamaduni, vipaji na taswira ya Tanzania nje ya mipaka yake.

Related Articles

Back to top button