Nyumbani

Viwanja 3 kuwaka moto Championship leo

LIGI ya Championship inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa Arusha, Mbeya na Mwanza.

Mbuni ya Arusha itakuwa mwenye wa Kengold ya Mbeya kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati TMA ya Arusha itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Nayo Pamba Jiji ya Mwanza itaikaribisha Polisi Tanzania ya Kimimanjaro kwenye uwanja wa Nyamagana.

Katika michezo mitatu iliyofanyika Machi 29, Pan African na Ruvu Shooting zimetoka sare ya mabao 2-2, Cosmopolitan imekubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Mbeya Kwanza wakati Copco imechapwa bao 1-0 na FGA Talents.

Kengold inaongoza Ligi ya Championship ikiwa na pointi 60 baada ya michezo 26 wakati Ruvu Shooting inaburuza mkia nafasi ya 16 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 27.

Related Articles

Back to top button