Nyumbani
Kivumbi Yanga vs Azam ngao ya jamii leo

NUSU fainali ya kwanza ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam inapigwa leo kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Katika nusu fainali ya pili Simba itaikabili Singida Fountain Gate Agosti 10 kwenye uwanja huo huo.
Michezo hiyo ya ngao ya jamii inafanyika kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Agosti 15.
Katika ufunguzi wa ligi hiyo Ihefu itakuwa mwenyeji wa Geita Gold kwenye uwanja wa Highland Estates, Mbeya huku JKT Tanzania ikiwa mgeni wa Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi wakati Dodoma Jiji itaikaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.