Muziki

Wiz Khalifa ashitakiwa kwa kuvuta bangi jukwaani

LOS ANGELES: RAPA kutoka nchini Marekani, Cameron Thomaz maarufu Wiz Khalifa ameshitakiwa nchini Romania baada ya kukamatwa na kukutwa na dawa za kulevya kinyume na sheria za nchi hiyo.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 36 alikutwa na bangi katika mikono yake asubuhi ya Julai 14 baada ya kutumia dawa hizo akiwa jukwaani kwenye tamasha la ufukweni huko Costinesti.

“Wakati wa tafrija iliyofanyika wakati wa tamasha la muziki lililofanyika katika eneo la mapumziko la Costinești, kaunti ya Constanța, Wiz Khalifa alikuwa na zaidi ya gramu 18 za bangi na akatumia akiwa jukwaani ikiwa katika umbo la sigara iliyosokotwa kiufundi,” Shirika la waendesha mashtaka dhidi ya uhalifu uliopangwa nchini humo DIICOT lilisema katika taarifa yake.

Hitmaker huyo wa ‘See You Again’ baada ya kuachiwa akaandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X akaomba msamaha kwa kuvuta sigara jukwaani, akisisitiza kwamba hakufanya hivyo kwa kudharau sheria za nchi hiyo wala kutoheshimu mamlaka.

“Onyesho la usiku wa jana lilikuwa la kushangaza. Sikuwa na maana yoyote ya kutoheshimu nchi ya Romania. Waliniheshimu sana na kuniacha niende. Nitarudi hivi karibuni,” aliandika.

Related Articles

Back to top button