Africa

Nyota 24 waitwa Twiga Stars kuivaa Togo

WACHEZAJI 24 wa timu ya taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Twiga Stars) wamechaguliwa kuingia kambini Novemba 22 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Togo Novemba 27, 2023.

Wachezaji hao ni magolikipa Najat Abasi, Husna Mtunda na Zulfa Makau huku mabeki wakiwa ni Juletha Singano, Anastazia Katunzi, Christer Bahera, Fatuma Issa, Vaileth Nicholaus na Happy Hezron.

Viungo ni Diana Mnali, Enekia Kasonga, Stumai Abdallah, Ester Mabanza, Joyce Lema, Janeth Christopher, Amina Bilali, Diana Lucas, Eto Hamisi, Aisha Juma na Winifrida Gerald.

Waliochaguliwa safu ya ushambuliaji ni Aisha Masaka, Donisia Minja, Oppa Clement na Jamila Rajabu.

Kuingia hatua hiyo Twiga Stars imetoa Ivory Coast wakati Togo imeiondosha Djibouti.

Related Articles

Back to top button