Africa

“CBE SA watakuja kukutana nacho”

DAR ES SALAAM: OFISA Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Ntime amesema wamerejea nyumbani na kujipanga kufanya balaa katika mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA ya Ethiopia.

Ntime amesema mechi waliyocheza ugenini haikuwa ya kuvutia kwa sababu ya uwanja haukuwa mzuri na hali ya hewa kutokuwa vizuri na lakini walifanikiwa kuanza vizuri safari yao ya makundi.

Bao pekee lilifungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube dakika ya 45 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Abebe Bikila jijini Addis Ababa, Ethiopia na mchezo wa marudiano utafanyika Jumamosi, Septemba 21, New Amaan Complex, Zanzibar.

Ofisa Mtendaji huyo ameliambia Spotileo kuwa wamecheza vizuri na kutengeneza nafasi ambazo hazikuweza kuzalisha mabao mengi lakini ana imani katika mchezo watakaocheza nyumbani kuna idadi kubwa ya mabao.

“Tunajivunia kupata ushindi huu wa bao 1-0 ugenini, sio mbaya sana, tunaenda Zanzibar, huko tunaenda kufanya balaa kwa CBE SA katika uwanja wa nyumbani,” amesema,

Ntime ameeleza kupata bao 1-0 ugenini imewapa urahisi wa kufanya vizuri mechi ya nyumbani kwa kuingia hatua ya makundi kwa idadi ya mabao mengi.

Related Articles

Back to top button