Africa

Mwigulu: Simba mmetuheshimisha

DODOMA: Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba amewapongeza wanafainali wa kombe la shirikisho barani Africa wekundu wa msimbazi Simba Sports Club kwa kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo na kumaliza nafasi ya pili kwa mara ya pili kwenye historia ya klabu hiyo.

Mwigulu ametoa pongezi hizo Bungeni jijini Dodoma leo na Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/26.

“Mheshimiwa Spika, niipongeze kwa dhati timu ya Simba kwa kutinga fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa mara nyingine tangu mwaka 1993. Mafanikio haya ya Simba yanatokana na juhudi kubwa ya uwekezaji inayofanywa na Rais wa heshima wa Timu hiyo Ndugu Mohamed Dewji”.

“Hii si tu inatoa heshima kwa Timu hiyo, bali pia inaitangaza nchi yetu katika ramani ya soka la kimataifa. Kusema kweli, Simba ya mwaka huu imepambana sana hasa ukizingatia kuwa Kocha bado anaijenga timu anayoitaka. Hivyo, nitoe pongezi kwa menejimenti ya timu pamoja na mashabiki wa Simba ambao wanaendelea kuwa mashabiki bora kabisa wakiongozwa na meneja wangu mimi (Striker), maarufu kama Semaji la CAF”.

Simba walicheza hatua hiyo na kumaliza nafasi ya pili huku ubingwa huo ukienda kwa RS Berkane baada ya matokeo ya jumla ya mabao 3-1

Related Articles

Back to top button