Burudani

Mstaafu Karume afunga ZIFF 2024

ZANZIBAR: Rais mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume amekabdhi tuzo ya mshindi wa jumla mwakilishi wa wa filamu ya Goodbye Julia, Joice Thomas.

TAMASHA la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limefungwa na Rais wa awamu ya sita, Dk Amani Abeid Karume usiku wa kuamkia leo.

Dkt Aman aliyekuwa ameongozana na mkewe alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa tamasha hilo lililoanza Agosti 1 na kuhitimishwa Agosti 4 visiwani Zanzibar.

Katika usiku huo wa tuzo Dk Karume alikabidhi tuzo ya filamu bora ya jumla kwa mwakilishi wa waandaaji wa filamu ya Goodbye Julia kutoka Sudan Kusini Joyce Thomas.

Dkt Amani amewataka waaanii na waandaaji pamoja na wadau wa sanaa kuongeza juhudi katika uandaaji wa filamu zenye maadili na kutopoteza utamaduni wa Mzanzibar.

Amesema Zanzibar imekuwa kitovu cha ushirikiano wa kimataifa katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu na tamasha hilo limekuwa kiungo bora katika suala hilo.

Mtendaji Mkuu wa Tamasha hilo, Joseph Mwale alisema katika siku nne ukiachia siku ya Zanzibar, kulikuwa na zaidi ya sinema 70 zilizooneshwa pamoja na makongamano yaliyojadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia ya filamu.

Tamasha la mwaka huu lilikuwa na kauli mbiu ya Kuhuisha likishikwa kwa mara ya kwanza na mtendaji kijana ambaye hajawahi kutokea katika miaka 27 ya uwepo wake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button