Mapenzi yamfanya Zuchu kuwa dansa

ZANZIBAR: Msanii wa Bongo Fleva nchini , Zuhura Othman maarufu kama ‘Zuchu’, aligeuka kuwa mtumbuizaji wa Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ katika usiku wa tuzo za Trace Award.
Katika hatua fulani, unaweza kusema kuwa wivu wa mapenzi ndio sababu ya Zuchu kuwa dansa wa Diamond Platnumz, kwani hapendi kuona mpenzi wake akicheza na wanawake wengine.
Waswahili husema kuwa “mtu chake”, hivyo Zuchu kucheza na Diamond Platnumz ni njia mojawapo ya kulinda penzi lake dhidi ya wanawake wanaomzunguka, hasa madansa wake.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, mitandao ya kijamii ilivuma kwa picha zinazoonyesha Diamond Platnumz akiwa na mwanamke mwingine, aliyesemekana kuwa mpenzi wake mpya.
Kupitia picha hizo, inawezekana kuwa Zuchu aliona ni bora kuchukua tahadhari kabla ya hatari.
Mbali na kupendeza na kuonekana kama malkia wa usiku huo, Zuchu aliitendea haki jukwaa akiwa na bwana Simba.
Hapo ndipo mashabiki walipogundua kuwa, hata akiacha kuimba, bado ana kipaji kingine cha kudansi.